Monday, June 13, 2016

HUU NDIO UKWELI KUHUSU USAFI WA MAZINGIRA

Mtoto akifanya usafi

Nimekuwa nikitafakari kwa kipindi kirefu kwa kutazama mtazamo na uelewa wa jamii  kuhusu usafi wa mazingira na kinachofanyika baada ya uchafuzi wa mazingira kutokea, nikajiuliza swali hili “nani mwenye jukumu la kutunza usafi wa mazingira?” bila shaka ukiwa mdau wa usafi wa mazingira, utajiuliza swali hili.Ikiwa hufahamu umuhimu wa usafi wa mazingira, utajua ni nani anahusika kutunza usafi wa mazingira ukiendelea kusoma makala hii.


Ili kuweka bayana suala hili la usafi wa mazingira, ni vyema tukajulishana au kukumbushana maana halisi ya neno “mazingira” …kwa uelewa wa kawaida, mazingira ni mjumuisho wa mambo yote yanayomzunguka binadamu, ukijumuisha mimea, wanyama na viumbe visivyo hai.Kwa lugha nyepesi, mazingira humtunza mwanadamu ukijumuisha mimea na wanyama.Hivyo, binadamu hupaswa kutunza na kuhifadhi mazingira  ili yamtunze, yatunze pia viumbe vingine vilivyo hali.
Binadamu anatajwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwa sababu ana utashi wa kujua mema na mabaya.Pia ndiye wa kwanza kuanzisha shughuli mbali mbali za kibiashara na kiuchumi katika mazingira yanayomtunza.Ikiwa sanjali na shughuli hizo, mwanadamu ana jukumu la kuhakikisha mazingira anayoishi hayaathiriwi na shughuli zake kwa hali moja au nyingine.
Nimezungumza kwa mapana sana, sasa niguse wahusika moja kwa moja.Kutokana na mgawanyiko wa majukumu ya kila siku,tofauti za hali kiuchumi, na fursa ya kuwepo kwa teknolojia ya viwanda kumetokea matabaka katika jukumu letu sote la kutunza usafi wa mazingira.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipothamini juhudi za watu wachache katika kuzingatia jukumu la ubinadamu la kutunza usafi wa mazingira.Mfano: vikundi vya kijamii, serikali kwa sehemu yake, Mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi.
Leo nitoe mfano wa shughuli zifanywazo na Shirika lisilo la Kiserikali “VoiceGiving” katika kusimamia usafi wa mazingira na kutoa elimu ya usafi wa mazingira jijini Dar es salaam-Tanzania. Shirika hili limenihamasisha sana kuhamasisha wengine kuhusu kuheshimu na kutunza mazingira yetu.

No comments:

Post a Comment